MJI ELDORET KUPANDISHWA HADHI AGOSTI 15

Ukabidhi wa hadhi ya jiji kwa mji wa Eldoret umeahirishwa kwa wiki moja hadi Agosti 15.
Gavana wa Uasin Gishu Jonathan Bii leo Jumatatu amesema hafla hiyo iliyokuwa ifanyike siku ya Alhamisi, Agosti 8 imeahirishwa baada ya kushauriana na serikali ya kitaifa.
Bii ameongeza kusema kuwa maandalizi yote ikiwa ni pamoja na kuutangaza mji huo kuwa wenye heri yanaendelea vizuri na wiki ya nyongeza itatoa muda zaidi wa kukamilisha maandalizi.
Rais William Ruto anatarajiwa kuongoza hafla ya kukabidhi hati ya jiji kwa gavana katika hafla itakayoandaliwa katika uwanja wa michezo wa Eldoret.
Imetayarishwa na Janice Marete