KWA NINI RUTO ASIIDHINISHE MSWADA WA FEDHA – AHMEDNASIR

Wakili Ahmednasir Abdullahi anasema Rais William Ruto hafai kuidhinisha Mswada wa Fedha wa 2024.
Katika taarifa , Ahmednasir amesema ni lazima Rais aurejeshe bungeni kwa marekebisho na kuongeza kuwa Ruto anahitaji kutafuta njia ya kuondoa ushuru unaowakandamiza wakenya ulioko katika Mswada huo.
Aidha amebainisha kuwa ni wakati wa Rais Ruto kusikiliza wito kutoka kwa Wakenya wa matabaka mbalimbali kwamba Mswada huo unakandamizana kwamba hatua hiyo haitamfanya rais Ruto kuonekana bali ni ishara ya uongozi bora.
Imetayarishwa na Janice Marete