RUTO AUNGA MKONO HATUA BIDEN YA KUMALIZA VITA VYA PALESTINA NA ISRAEL
Rais William Ruto ameunga mkono hatua ya Rais wa Marekani Joe Biden akitaka kusitishwa kwa mzozo unaoshamiri kati ya Israel na Palestina.
Katika mtandao wake wa X, Ruto amebainisha kuwa mpango huo ulioanzishwa kwa pamoja na Marekani, Qatar na Misri, utafungua njia kwa ajili ya ujenzi mpya wa Gaza.
Ruto, ambaye yuko nchini Korea, ameongeza kuwa mpango huo pia utakuwa msingi wa usitishaji vita wa kudumu na utekelezwaji wa suluhu ya mataifa mawili, huku Israel na Palestina zikishirikiana pamoja, na kuchangia kuwepo kwa utulivu na haki.
Imetayarishwa na Janice Marete.
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































