NITABADILISHA AFC ASEMA AMBANI
Mwenyekiti mpya wa AFC Leopards, Boniface Ambani anasema anataka kukumbukwa kama kiongozi aliyekuja na kubadilisha mambo makubwa kwa manufaa ya timu, kufikia wakati atakapokuwa akipeana uongozi miaka ya baadaye.
Ambani anatarajiwa kuchukua wadhifa huo rasmi leo kutoka kwa mwenyekiti anayemaliza muda wake Dan Shikanda, kufuatia kuchaguliwa kwake Jumapili iliyopita.
Ambani ameapa kuhakikisha Leopards inasikika kwenye anga ya kimataifa ikishindana na wababe wa Afrika.
Ambani hata hivyo anajua kwamba ufadhili utakuwa Muhimu ikiwa ni kufikia ndoto zake.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































