#Business

SERIKALI KUPUNGUZA UTEGEMEZI KWA WAKOPESHAJI KUTOKA NJE

Kama njia mojawapo ya kuhahakisha kuwa serikali kuu haitalemewa na mzigo wa deni la umma na kupunguza utegemezi wake wa wakopeshaji kutoka nje, wizara ya fedha sasa ina mkakati mpya ambapo inapanga kukopa fedha kutoka kwa wakopeshaji wa ndani kwa asilimia kubwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya serikali kuu na ile ya kaunti.

Akizungumza na wanahabari Waziri wa fedha John Madi amebainisha kuwa serikali inalenga kupata mikopo kwa asilimia 25 pekee kutoka nje na asilimia 75 kutoka kwa wakopeshaji wa ndani katika kipindi kijacho. Mbadi aidha ametaja kuwa hilo limeafikiwa ili kuinasua nchi kutokana na hatari na masharti yanayotokana na mikopo ya umma katika kipindi fulani.

Kulingana na Hazina ya Kitaifa, jumla ya deni la umma lilifikia takriban shilingi trilioni 10.5 kufikia mwishoni mwa mwezi Juni 2024, ambapo deni la ndani lilikuwa asilimia 51.1 huku deni la nje likiwa asilimia 48.9.

Vile vile imebainika kuwa deni la kimataifa linachangia asilimia 53.9 ya deni la nje, likionyesha mkakati wa nchi wa kuongeza matumizi ya ufadhili wa masharti nafuu na kupunguza  matumizi ya deni la kibiashara.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

SERIKALI KUPUNGUZA UTEGEMEZI KWA WAKOPESHAJI KUTOKA NJE

MUTURI HAKUFUTWA, OWINO ADAI

SERIKALI KUPUNGUZA UTEGEMEZI KWA WAKOPESHAJI KUTOKA NJE

JESHI LA SUDAN LAAPA KUISAMBARATISHA RSF

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *