RAILA APOKELEWA JUMBA LA RHODES CHUONI OXFORD

Kiongozi wa Azimio la umoja Raila Odinga aliyeondoka nchini kuelekea Uingereza siku ya Jumatano akiandamana na katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna na mbunge wa Nyado Jared Okello amezuru jumba la Rhodes katika chuo kiku cha Oxford.
Kwenye ujumbe kupitia akaunti yake ya X, Raila amesema amekaribishwa na kaimu balozi wa Kenya nchini Uingereza Edwin Afande.
Kwa mujibu wa taarifa ya Azimio kupitia kwa msemaji wake Dennis Onyango imesema Raila yuko Uingereza baada ya kualikwa na jamii ya Waafrika nchini humo, ambako anatarajiwa kuhutubu katika kongamano la kila mwaka lenye kauli mbiu FORGING AFRICA’S FUTURE.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa