KENYA YAPOTEZA MABILIONI KATIKA KASHFA YA MAFUTA
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Nancy Gathungu amesema kuwa Wakenya walipoteza mabilioni katika kashfa ya mafuta ya kupikia iliyoungwa mkono na Serikali,
Gathungu sasa anatoa wito kwa mashirika ya uchunguzi kuhitimisha uchunguzi wao ili kuruhusu kufunguliwa mashtaka kwa watu na mashirika yenye yatakayopatikana na hatia
Katika matokeo yake ya hivi punde ya ukaguzi maalum kuhusu kashfa ya mabilioni kufuatia ombi la Kamati ya Bunge ya Kitaifa ya Uhasibu wa Umma kuhusu mpango wa Shilingi bilioni15, Gathungu ameweka wazi jinsi Shirika la Kitaifa la Biashara la Kenya (KNTC) lilivyovuruga, na kuwaacha Wakenya wakihangaika na bei ya juu. ya mafuta ya kupikia.
Ripoti hiyo inasema serikali ilitumia Shilingi bilioni14.45 kuagiza mafuta ya kupikia milioni 2,807,806 milioni 20 ambapo kati ya hizo Shilingi bilioni12.05 pekee ndizo zililipwa.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































