MIA MBILI YA MAUTI

Mwanaume mwenye umri wa miaka 25 amefariki kufuatia mzozo wa shilingi 200 katika soko la Garissa Lodge, eneobunge la Kisumu ya kati.
Inaripotiwa kuwa mzozo huo ulitokea baada ya wanaume hao wawili kuuza kiatu na kwamba walipaswa kugawana mapato.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kisumu ya kati Peter Mulai, mtuhumiwa, kwa jina Nicholas Otieno, amempiga mwerevu upande wa kushoto, jambo lililosababisha kuanguka nyuma na kugongwa kichwa chake na kukumbizwa hospitalini, ambapo amethibitishwa kufariki akiwa hospitalini kutokana na majeraha makubwa kichwani.
Baada ya kusikia kuhusu kifo chake, wanajamii waliokasirika walimshambulia Otieno kwa kipigo kikali hadi alipokuwa karibu kufa kabla ya polisi kuingilia kati.
Otieno kwa sasa anashikiliwa chini ya ulinzi wa polisi katika Hospitali ya Kaunti ya Kisumu akitarajiwa kufikishwa mahakamani kwa mashtaka ya mauaji atakapopona.
Imetayarishwa na Janice Marete