MIMI NA WANDANI WANGU TUNALENGWA- GACHAGUA

Naibu Rais Rigathi Gachagua amedai kwamba afisa wa zamani wa idara ya ujasusi wa kitaifa NIS ambaye aliajiriwa na Gachagua baada ya kutimuliwa na idara hiyo alipigwa risasi na kujeruhiwa begani alipokuwa njiani kuelekea kazini katika mtaa wa Karen jijini Nairobi.
Akizungumza kwenye mahaojiano na vituo vya redio vinavyopeperusha matamgazo kwa lugha za eneo la Mlima Kenya, Gachagua amedai kuwa afisa huyo alipigwa risasi na muuaji wa kukodishwa na kwamba hadi sasa hajakamatwa wala kisa hicho kuchunguzwa.
Aidha, Gachagua amedia kwamba mawasiliano yake ya simu yamekuwa yakifuatiliwa kwa lengo la kumdhibiti kisiasa, na kwamba wandani wake wa kisiasa vile vile wanalengwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa