#Business

WITO WA KRA

Mamlaka ya kukusanya ushuru nchini KRA imetoa wito kwa walipa kodi wote waliosajiliwa kusasisha maelezo yao ya usajili kwenye mfumo wa iTax.

Katika notisi ya leo hii, Mamlaka hiyo imesema limeanzisha zoezi la kina la kusafisha data kwa maelezo yote ya usajili ya nambari za kibinafsi za walipa kodi (PIN).

Maelezo yatakayosahihishwa ni pamoja na nambari ya simu, anwani ya mahali ulipo, anwani ya barua pepe, eneo halisi la biashara, hali ya makaazi na uelekezi au ushirikiano unaofanywa miongoni mwa zingine.

Juhudi hizo kulingana na KRA ni sehemu ya mkakati wake wa kurahisisha utendakazi na kuboresha ufanisi ndani ya mfumo wa usimamizi wa ushuru.

Ili kuwezesha mchakato wa kusasisha, walipa kodi wanatakiwa kuingia kwenye mfumo wa iTax, kuthibitisha nambari zao za simu zilizosajiliwa na kusasisha maelezo yoyote ya mawasiliano yasiyo sahihi.

iTax ni mfumo uliotengenezwa na wakala ili kuboresha ufanisi na inaruhusu mtu kusasisha maelezo yake ya usajili wa ushuru, faili za marejesho ya ushuru na kusajili malipo yote ya ushuru.

Ili kufikia mfumo wa iTax, mtu anatakiwa kuingia kwa kutembelea itax.kra.go.ke na kufuata madokezo.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

WITO WA KRA

‘MAANDAMANO YA PUNDA’ LAMU

WITO WA KRA

KENYA MBIONI KUMALIZA EUROBOND

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *