#Local News

UASIN GISHU YAUPA KIPAUMBELE UJENZI WA BARABARA

Kaunti ya Uasin Gishu imetoa kipaumbele kwa ujenzi wa barabara kwenye mwaka wa kifedha wa 2025-26 ili kurahisisha usafiri katika maeneo ya mashinani, sekta hiyo ikitengewa shilingi bilioni 2.5 kwenye bajeti yake.

Akiwasilisha makadirio ya bajeti bungeni, waziri wa fedha kwenye serikali ya kaunti hiyo Micah Rokony, amesema katika kipindi cha miaka 2 iliyopita, kaunti hiyo imekuwa ikijishughulisha pakubwa na masuala ya afya.

Sekta ya afya hata hivyo imetengewa shilingi bilioni 2.4, milioni 60 zikirataibiwa kutumika katika ujenzi wa hospitali ya kaunti ndogo ya Moiben.

Imetayrishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *