WATATU WAFARIKI KWENYE MMOMONYOKO BUNGOMA

Watoto watatu wa familia moja kutoka Kijiji cha Chesiywo Wadi ya Chesikaki eneobunge la Mlima Elgon Kaunti ya Bungoma wameaga dunia baada ya kufunikwa na mmomonyoko wa udongo kufuatia mvua kubwa iliyoshuhudiwa usiku wa kuamkia leo.
Wakaazi wanasema watatu hao waliokuwa wamelala kwenye nyumba moja wamefariki papo hapo, huku wazazi wao wakipelekwa katika hospitali ya rufaa ya Bungoma.
Aidha wametoa wito kwa idara ya majanga Kaunti ya Bungoma kuzuru eneo hilo na kutoa msaada wa vyakula huku wakitoa wito kwa serikali kuwatengea maeneo mbadala ili kuwaepusha na maafa zaidi.
Naibu Chifu wa kata ndogo ya Chemondi, Martin Naibei amethibitisha kisa hicho na kuwataka wananchi kuhamia sehemu salama ili kuepuka majanga mengine kutokea
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa