HONGERA POLISI BULLETS KWA KUFIKA FAINALI; KOCHA ODEMBA
Kocha mkuu wa Kenya Police Bullets fc, Beldine Odemba amesifu wachezaji wake kwa kufika fainali ya kuwania kufuzu kwa ligi klabu bingwa afrika ya Wanawake ya Cecafa lakini anasema inauma kwamba walikosa tiketi hiyo.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake nchini walifungwa 1-0 na CBE ya Ethiopia katika fainali jana mjini Addis Ababa, huku kipigo hicho kikimaliza matumaini yao ya kushiriki Ligi klabu bingwa afrika ya CAF kwa mara ya kwanza.
Odemba ambaye aliibuka kocha bora wa mashindano hayo amejizatiti kuelekeza nguvu kwenye ligi ya humu nchini mara moja huku wakilenga kuhifadhi taji lao waliloshinda msimu uliopita kwa mara ya kwanza na pia bila kupoteza mechi hata moja.
Mlinda lango wa Bullets Annedy Kundu alichaguliwa kuwa kipa bora wa michuano hiyo.
CBE itawakilisha eneo la Cecafa katika Ligi klabu bingwa ya Wanawake ya Caf inayotarajiwa kuanza baadaye mwaka huu.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































