#Local News

PITISHA BAJETI KOMBOA KENYA KUTOKA KWA MADENI ASEMA KIMANI KURIA

Wizara ya fedha imeitaka bunge la kitaifa kupitisha mswada wa fedha bila kuufanyia marekebisho ili kuwezesha serikali kulipa madeni ambayo yamefikia shilingi trilioni 11.2

Kwa mujibu wa Waziri wa fedha Njuguna Ndugu ni kupitia kodi kenya itaweza kupunguza madeni inayodaiwa na mataifa mengine

Tayari kamati ya fedha na mipango  ya bunge la kitaifa imeanza kuandika ripoti yake ambayo inatarajiwa kuwasilisha bungeni wiki ijayo

Mbunge wa Molo Kimani Kuria ambaye ni mwenyekiti wa kamati huyo ameahidi kwamba maoni ya wakenya sharti yapewe kipaumbele katika ripoti hiyo

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *