KIKOSI CHA KENYA CHAWASILI MOROCCO TAYARI KWA OLYMPIKI.

Timu Za Kenya Za Voliboli Ya Ufukweni(Beach Volleyball) Zilisafiri Kwa Makundi Mawili Kwa Michezo Ya Afrika Ya Mpira Wa Wavu Ya Ufukweni Kuwania Kufuzu Kwa Olimpiki, Mechi Zilizo Anza Jana Mjini Tetouan, Morocco.
Kundi La Kwanza La Naomi Too Na Brian Melly Pamoja Na Mkuu Wa Ujumbe Neddy Kilimo Liliondoka Jana Asubuhi Huku Kundi La Pili La Sogora Gaudencia Makokha Na Edward Kibet Pamoja Na Benchi La Ufundi Likiondoka Jana Jioni Kwa Mashindano Hayo Ya Siku Tano.
Kwa Upande Wa Timu Ya Wanawake, Gaudencia Makokha Atashirikiana Na Naomi Too Katika Kuwania Tiketi Ya Olimpiki Kwa Mara Ya Pili Mfululizo Baada Ya Hapo Awali Kushirikiana Na Braxides Agala Kutwaa Medali Ya Fedha Katika Michezo Ya Afrika 2019 Na Pia Katika Michezo Ya Olimpiki Ya Tokyo 2020.
Upande Wa Wanaume Brian Melly Na Edward Kibet Watakuwa Wakilenga Kufuzu Kwa Olimpiki Kwa Mara Yao Ya Kwanza.
Timu Hizo Mbili Zimekuwa Katika Kambi Ya Makazi Katika Hoteli Ya Flamingo Beach Mjini Mombasa.
Imetayarishwa na Nelson Andati.