UTEUZI WA MAKAMISHNA WA IEBC WAANZA

Zoezi la kuwahoji wawaniaji wanaotaka kuwa makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC limeanza hii leo, ikiwa ni siku moja baada ya mahojiano ya wawaniaji wa uwenyekiti wa tume hiyo kukamilika.
Wa kwanza kuhojiwa hii leo ni Abduba Molu, akisisitiza haja ya tume hiyo kuwa uhuru na kutekeleza majukumu yake bila miingiliano ya kisiasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa