KFS NA MAAFISA WENGINE WAENDELEZA UPANZI WA MICHE KATIKA MSITU WA KITALE TOWNSHIP
Maafisa wa shirika la misitu KFS ,wale wa idara ya polisi na magereza Pamoja na wa kulinda Wanyama pori, maafisa wa utawala na wale wa serikali ya kaunti ya transnzoia wameendeleza juhudi za kupanda miche katika msitu wa Kitale Township kukabili mabadiliko ya hali ya anga.
Kamishina wa kaunti hiyo Gideon Oyagi na afisa wa kusimamia misitu katika kaunti hiyo Eli Tinda wanasema msitu huo wa ekari 402 ambao miti ilikatwa kuwa kuni ili kutumika kwa ajili ya gari la moshi wakati wa ukoloni haukutunzwa hivyo basi kuadhiri ekari takribani 300 za msitu huo.
Kamanda wa polisi kaunti hiyo Jeremiah Kosiomo na kamanda wa polisi wa utawala Simon Njenga wamewaonya wanataoharibu misitu kuwa watachukuliwa hatua kisheria.
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































