KUMBANDUA GACHAGUA KUTAUNDA SHUJAA KUTOKA KWA ‘MBABE WA KABILA’ – SENETA KAJWANG’
Seneta wa Homa Bay Moses Kajwang’ amesema kuwa kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua mamlakani ni hatua mbaya ya kisiasa ambayo inafaa kuepukwa.
Kwa maoni yake, kumtimua Gachagua afisini kutakuwa na athari mbaya kwa hali ya kisiasa inayompa umaarufu usio na msingi.
Akihojiwa katika kituo kimoja cha runinga humu nchini Kajwang’ amebainisha kuwa kauli za Gachagua za siasa za kikabila zitaimarishwa mara tu atakapotimuliwa afisini.
Kwa upande wake, Mbunge wa Mbeere Kaskazini Geoffrey Ruku amebainisha kuwa kuna nia halali ya kumshtaki Gachagua, akisema hakuna hoja iliyowasilishwa mbele ya Bunge la Kitaifa.
Tetesi za kumwondoa madarakani kiongozi huyo zimekuwa zikiongezeka huku misimamo michache ya kisiasa ikidaiwa kuandaa njama ya kutaka abanduliwe kwenye wadhifa wa naibu wa rais na vile vile naibu mwenyekiti wa chama cha UDA.
Ripoti zimedokeza kuwa hatua ya kumtimua Gachagua ni kwa misingi ya kuhujumu wadhifa wa urais
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































