NIKO TAYARI KUINGIA AUC, ODINGA
Ikiwa ni chini ya wiki moja kabla ya uchaguzi wa uwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika AUC kuandaliwa, waziri mkuu wa zamani Raila Odinga ambaye pia ni moja kati ya wawaniaji 3 kwenye kinyang’anyiro hicho, amesema atakubali matokeo ya uchaguzi huo.
Akizungumza katika kongamano la viongozi wanawake wa chama cha ODM jijini Nairobi, Odinga hata hivyo amesema amejiandaa vya kutosha kwa ajili ya kuibuka mshindi.
Aidha, Odinga ameitaka serikali kukomesha visa vya utekaji nyara.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































