USHINDI UMEIMARISHA KIKOSI
Kocha mkuu wa KCB RFC kikosi chao cha raga ya wachezaji saba kila upande Andrew Amonde anasema ushindi wa Kabeberi Sevens umeongeza ushindani mzuri miongoni mwa wachezaji wake wanapoelekea kwa mikondo miwili ya mwisho ya msururu wa kitaifa wa raga ya wachezaji saba.
Amonde alisema kuwa kila mchezaji ana ari na anataka kuwa sehemu ya timu itakayoshinda shiriki mkondo wa Driftwoods Sevens wikendi hii na mkondo wa mwisho mjini Nakuru.
Mabingwa hao watetezi waliwashinda Menengai Oilers 29-7 katika fainali ya Kabeberi Sevens lakini Amonde anaamini bado wanahitaji kufanyia kazi safu yao ya ulinzi.
KCB kwa sasa wako katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa msururu huo wa kitaifa na alama 67, sita nyuma ya Kabras walio nafasi ya pili na nane nyuma ya vinara Kenya Harlequins, na nahodha huyo wa zamani wa Shujaa anaamini wana kile kinachohitaji kutetea ubingwa wao.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































