MWINAMO AWASUTA GREEN COMMANDOS KWA KULIALIA

Mkufunzi Mkuu Wa Timu Ya Shule Ya Wavulana Ya Musingu Maarufu The Scorpion Ambayo Iliibuka Mshindi Kwenye Michuano ya Shule Za Upili Kakamega na Sasa Itaakilisha Kaunti Hiyo Kwenye Michuano ya Shule Za Upili Ngazi Ya Ukanda Wa Magharibi, Brendan Mwinamo Ametaja Hatua Ya Timu Ya Kakamega School The Green Commandos Kila Mara Kukata Rufaa Inaposhindwa Kama Ya Kujidunisha.
Akizungumza Na Michezo Mashinani, Mwinamo Anasema Hulka Ya Timu Hiyo Kukataa Rufaa Inaposhindwa Imekuwa Ya Kukera Mno Akidokeza Kuwa Yeye Mwenyewe, Amekuwa Mwalimu Wa Muda Mrefu Wa Shule Ya Kakamega Na Pia Mkufunzi Wa Timu Hiyo Na Hana Uhasama Wowote Na Shule Hiyo.
Imetayarishwa na Nelson Andati