#Sports

WAKENYA WATIA FORA DIAMOND LEAGUE

Nyota wa Kenya wa mbio za masafa ya kati waliang’aa uwanjani katika mashindano ya Diamond League jijini Stockholm uswidi hapo jana, Emmanuel Wanyonyi akiwa gumzo kwa kukimbia kwa kasi ya ajabu ya 1:41.95 na kushinda mbio za mita 800 kwa wanaume — muda bora zaidi duniani kwa mwaka huu.

Akiwa na umri wa miaka 20 pekee, Wanyonyi sasa ni mwanamme wa kwanza msimu huu kuvunja kizuizi cha dakika 1:42, akikariri ujio wake na kutamalaki mbio hizo.

Ushindi huo vile vile ni wake wa pili mfulululizo katika mashindano ya Diamond League, baada ya ushindi mwingine siku chache zilizopita jijini Oslo ambako aliandikisha muda wa dakika 1:42:78

Djamel Sedjati wa Algeria alimaliza wa pili kwa 1:42.27, huku Mwamerika Josh Hoey akiandikisha muda wa dakika 1:42.43 na kumaliza wa tatu katika mbio hizo za mita 800 zilizokuwa zenye ushindani zaidi msimu huu.

Kwa upande wa akina dada, mkenya mwingine Mary Moraa alisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kumaliza wa pili ikiwa ni rekodi yake bora ya msimu kwa dakika 1:57:83, nyuma ya Mwingereza Georgia Hunter-Bell.

Prudence Sekgodiso wa Afrika Kusini alimaliza wa tatu.

Imetayrishwa na Antony Nyongesa

WAKENYA WATIA FORA DIAMOND LEAGUE

STARLETS WANG’AA DHIDI YA BURUNDI

WAKENYA WATIA FORA DIAMOND LEAGUE

HUSTLER YADHIBITIWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *