MWANASHERIA MKUU DORCAS ODUOR NA BEATRICE ESIKUL WAAPISHWA

Mwanasheria mkuu Dorcas Oduor na Waziri wa jumuiya ya afrika mashariki na maeneo kame Beatrice Askul wanaapishwa hii leo katika ikulu ya Nairobi katika hafla inayoongozwa na Rais William Ruto.
Katika hafla hiyo rais Ruto ameeleza matumaini yake kwa mwanasheria mkuu kwa kuwa kulingana naye ana tajriba ya kutosha ya kuimarisha utendakazi katika afisi ya mwanasheria mkuu.
Imetayarishwa na Janice Marete