WANAHARAKATI WATAKA UTEUZI WA JOHO UBATILISHWE

Kundi moja la wanaharakati limeelekea mahakamani kupinga uteuzi wa Ali Hassan Joho kuwa Waziri wa madini na raslimali za majini, likisema kamati ya uteuzi katika bunge la kitaifa lilipuuza notisi kadhaa zenye ushahidi kwamba Joho hakufaa kuteuliwa.
Kulingana na kundi hilo, Joho hakufaa kuidhinishwa kwa misingi kwamba stakabadhi hitajika za masomo, na sasa wanaitaka mahakama kutoa agizo la kumzuia kutekeleza majukumu yake kama Waziri, na kufutilia mbali uteuzi wake.
Jaji Lawrence Mugambi amesema atatoa mwelekeo kuhusu kesi hiyo tarehe 17 mwezi Oktoba.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa