MANCHESTER UNITED KUVAANA NA ASENALI KATIKA MCHEZO WA UFUNGUZI
Liverpool wataanza kutetea taji lao la Ligi ya Premia wakiwa nyumbani dhidi ya Bournemouth Ijumaa, Agosti 15 huku Arsenal wakimenyana na Manchester United katika mchuano mkali wikendi ya ufunguzi.
Mabingwa wa Arne Slot wana nafasi ya kupata alama za kwanza za msimu mpya huko Anfield wanapozindua kampeni ya 2025/26.
Kufuatia mchezo wa Bournemouth wana mechi ngumu huko Newcastle na nyumbani kwa Arsenal.Mechi ya kwanza ya Thomas Frank kama bosi wa Tottenham itashuka Agosti 16 nyumbani dhidi ya Burnley iliyopanda daraja, huku Sunderland ikirejea kwenye ligi kuu dhidi ya West Ham siku hiyo hiyo.
Wageni wapya wa tatu, Leeds, watacheza na Everton Jumatatu, Agosti 18.
Manchester United inayonolewa na Ruben Amorim, ambayo itatamani sana kuanza vyema baada ya kampeni mbaya ya ligi msimu uliopita, imepewa mtihani mzito katika mchezo wa nyumbani dhidi ya Arsenal mnamo Agosti 17.
Siku ya mwisho ya msimu itakuwa Mei 24, na mechi ikiwa ni pamoja na Manchester City dhidi ya Aston Villa.
Imetayrishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































