MTU MMOJA AMEFARIKI NA WENGINE 3 KUJERUHIWA KATIKA AJALI BARABARA YA KAGIO-BARICHO
Mtu mmoja amefariki na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya barabara eneo la Thumaita Kagio-Baricho huko Ndia, Kaunti ya Kirinyaga.
Kulingana na Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Kirinyaga Magharibi (Ndia) Moses Koskei, ajali hiyo imetokea wakati gari hilo lilibingiria mara kadhaa kabla ya kutua kwenye mtaro.
Kulingana na mkuu wa polisi, gari hilo lilikuwa likiendeshwa na muuguzi katika Kituo cha Afya cha Baricho.
Imetayrishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































