MWANAUME AMUUA MPENZIWE KISHA AKAJISALIMISHA KWA POLISI

Mwanaumwe mwenye umri wa miaka 24 amekamatwa na polisi eneo la makutano baada ya kudaiwa kumuua mpenziwe mwenye umri wa miaka 22 kwa kumdunga kisu mara kadhaa mwilini.
Kwa mujibu wa polisi katika kituo cha Kapenguria mwanaume huyo alipiga simu asubuhi leo kwa lengo la kujisalimisha kwa polisi akisema kwamba alikuwa ametekeleza kitendo hicho katika kijiji cha mawingo road viungani mwa mji wa makutano.
Jamaa huyo amejisalimisha mikonon I mwa polisi akikiri kumuua mpenziwe baada ya mgogoro kuzuka baina yhao usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa majirani jamaa huyo wanasema kwamba kumekuwapo na ugomvi baina ya wapenzi hao tangu jana ambapo mwanaume huyo alilazimika kulala nje usiku kucha baada ya kufungiwa mlango.
Mwili wa marehemu umepelekwa katika hifadhi yama Kapenguria huku mshukiwa akitarajiwa kufikishwa mahakamani.
Imetayarishwa na: Janice Marete