TIMU YA ASTON VILLA IMESHIRIKI MASHINDANO YA KLABU BINGWA BARANI ULAYA KWA MARA YA KWANZA
Klabu ya Aston Villa ni miongoni mwa timu ambazo zimecheza kwa mara ya kwanza katika ligi ya klabu bingwa barani Ulaya.
Aston Villa hapo jana waligaragazana na timu ya Uswizi ya Young Boys na kuwachapa kichapo takatifu cha mabao 3-0 ugenini.
Villa walijikatia tiketi ya kushiriki mashindano hayo baada ya kumaliza katika nafasi ya 4 msimu uliopita wa mwaka 2023/24.
Kocha wa Aston Villa Unai Emery ameelezea matumaini yake kufanya vyema kwenye mechi za klabu bingwa Ulaya baada ya kupata ushindi wake wa kwanza na klabu hiyo kwenye dimba la kutwaa taji la bara ulaya.
Emery amesema kikosi chake kina motisha na atatumia ujuzi wake kama kocha kuhakikisha Aston Villa inatoa ushindani mkubwa katika mechi zao zijazo.
Imetayarishwa na Kennedy Osoro
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































