KeNHA KUFUNGA BARABARA ENEO LA GITARU, KIAMBU

Shughuli za usafiri zimeratibiwa kutatizika kwenye barabara kuu ya Nakuru kuelekea Nairobi Jumatano ijayo, baada ya mamlaka ya barabara kuu KeNHA kutangaza kwamba itafunga barabara hiyo katika eneo la Gitaru kaunti ya Kiambu ili kuruhusu ujenzi wa Gitaru interchange.
Kupitia taarifa, KeNHA imesema magari yanayotokea upande wa Nakuru yatachukua barabara ya Regen/Magara na kujiunga na barabara ya Southern Bypass.
Tangazo hili limejiri muda mfupi baada ya watu 10 kuaga dunia katika eneo la Gitaru, madereva wakiilaumu KeNHA kutokana na ajali hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa