UGONJWA TATA KISII WAANZA KUBAINIKA
Huenda suluhu likapatikana kwa ugonjwa usiojulikana ambao umezua hofu katika katika eneo la South Mugirango kaunti ya Kisii, bada ya uchunguzi kuuhusisha na maji machafu.
Kupitia taarifa, katibu katika wizara ya afya Mary Muthoni amesema uchunguzi wa sampuli zilizokusanywa zimeonyesha uwepo wa kinyesi kwenye mojawapo ya visima vya maji eneo hilo.
Huku akisema uchunguzi unaendelea, Muthoni amewataka wakazi kusitisha matumizi ya maji kutoka kwenye kisima hicho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































