AFISA WA POLISI MUKHWANA RUMANDE SIKU 21 ZAIDI

Mahakama imeagiza kuzuiliwa kwa siku 21 zaidi afisa wa polisi James Mukhwana, aliyekiri kumtesa mwalimu na bloga Albert Ojwang kwa maagizo ya OCS wa kituo cha polisi cha Central Samson Taalam na naibu inspekta mkuu wa polisi aliyejiondoa kwa muda Eliud Lagat.
Kwenye uamuzi wake, hakimu Robinson Ondieki amekubaliana na sababu za upande wa mashtaka uliiomba muda huo ili kuendeleza uchunguzi.
Uamuzi huo umetolewa licha ya mawakili kupinga ombi la mamlaka ya IPOA, wanayosema haina mamlaka ya kuwafungulia mashtaka maafisa wa polisi bali ni jukumu la afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma.
Imetayrishwa na Antony Nyonesa