GAVANA KAHIGA, SUDI WAMJIBU MALALA

Baadhi ya viongozi wa eneo la mlima Kenya wanadai kwamba umaarufu wa chama tawala cha UDA umeanza kufifia katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa Katibu mkuu wa chama cha jubilee Jeremiah Kioni malumbano yanayoendelea ndani ya chama hicho ni ishara tosha kwamba huenda chama hicho kikasambaratika kabla ya uchaguzi wa 2027
Katika mahojianao na kituo kimoja cha runinga humu nchini kioni anasema kwamba baadhi ya viongozi na wakaazi wa mlima kenya wanahisi kutelekezwa na uongozi wa chama hicho.
Kauli hii inajiri wakati ambapo tofauti zimeibuka wazi katika chama hicho baada ya katibu mkuu wa UDA Cleophus Malala kutishia kuwaadhibu baadhi ya viongozi katika mrengo huo wanaokosea heshima wakuu chamani.
Walioorotheshwa kupewa adhabu ni mbunge wa Githunguri Gathoni wa Muchomba, gavana wa Nyeri Mutahi Kaiga na mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi.
Hata hivyo sudi na kaiga wamepuuzilia mbali kauli ya Malala na hata kutishia kwamba wanaweza kumtimua katika wathifa wa katibu mkuu wa chama hicho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa