MBIO ZA MTOZA USHURU
Mamlaka ya kukusanya Ushuru KRA ina kibarua cha kukusanya kodi ya Shilingi bilioni 567 ifikapo mwisho wa mwezi Juni mwaka huu ili kuafikia lengo lake la kukusanya mapato kwa mwaka wa kifedha.
Kwenye taarifa, mapato halisi ya hazina ya kitaifa ya mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu inaonyesha kuwa mapato ya kodi yaliongezeka kwa asilimia 9.5 ambayo ni sawa na shilingi bilioni 183.1.
Hata hivyo, kiwango hicho cha mapato ya hazina ya kitaifa kina mapungufu kwani KRA hataafikia lengo lake la kila mwaka la shilingi trilioni 2.4 kwa mwaka wa kifedha 2023/2024.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































