MIKOPO GHALI: CBK KUJIBU MBELE YA BUNGE

Wafanyabiashara bado wanakabiliwa na gharama kubwa ya mikopo licha ya Benki Kuu ya Kenya (CBK) kupunguza kiwango cha riba.
Kutokana na hali hiyo, Gavana wa CBK, Kamau Thugge, anatarajiwa kufika mbele ya Bunge la Kitaifa leo kueleza sababu za benki za biashara kutozingatia hatua hiyo.
Wakati huo huo, Kamati ya Fedha na Mipango ya Kitaifa, inayoongozwa na Mbunge wa Molo, Kimani Kuria, itamhoji Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji (CMA), Wycliffe Shamiah, kuhusu ushiriki wa NSSF katika biashara ya hati fungani, ambayo huenda ilisababisha hasara ya fedha za umma.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi