MUUNGANO WA KNUT BUSIA WATANGAZA MGOMO
Chama cha walimu KNUT tawi la Busia kimewaonya wanachama wake dhidi ya kuripoti kazini tarehe 26 agosti wanafunzi watakaporejea shuleni kwa muhula wa tatu kufuatia hatua ya serikali kutotimiza matakwa yao.
Katibu mkuu wa KNUT tawi la Busia Patrick Mulumba anasema kuwa kwa kauli moja wamekubaliana kutorejea kazini hadi pale serikali itatekeleza matakwa yao kama vile kuwaajiri walimu wa sekongdari ya msingi JSS kwa mikataba ya kudumu na pensheni.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































