UWANJA WA KASARANI UKO TAYARI KWA CHAN
Waziri wa Michezo Salim Mvurya amethibitisha kua uwanja wa Moi, Kasarani, sasa uko tayari kuandaa Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) ya 2025 inayotarajiwa kufanyika Agosti.
Mvurya alitoa taarifa hiyo baada ya kupokea rasmi kiwanja hicho kutoka kwa mkandarasi aliyepo eneo la tukio, ikiwa ni hatua muhimu katika maandalizi ya Kenya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo pamoja na Uganda na Tanzania.
Uwanja huo ulikuwa umefungwa kwa ukarabati tangu mwaka jana. Makabidhiano hayo yanaashiria kuwa Kasarani sasa iko tayari kukidhi viwango vya kimataifa kabla ya michuano hiyo ya hadhi ya juu ya bara.
Mvurya alifichua kuwa atapitisha mara moja funguo za uwanja kwa Kamati ya Maandalizi ya Ndani ya CHAN (LOC) ili kuanza mipango ya uendeshaji na vifaa kabla ya kazi ya bara.
Wakati huo huo, Mvurya alitoa wito kwa wananchi kutunza miundombinu iliyokarabatiwa na kujengwa upya.
Alionya dhidi ya vitendo vya uharibifu akisisitiza kuwa uharibifu wa miundombinu utasababisha ukarabati wa gharama kubwa na kufifia kwa bajeti.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































