TUSULUHISHE KESI NDOGO NDOGO NJE YA MAHAKAMA
Wakaazi Kaunti ya Homa Bay wamehimizwa kukumbatia njia mbadala katika kusuluhisha kesi mbali mbali ili kupunguza mrundiko wa kesi mahakamani na kuharakisha waliokosewa kupata haki.
Jaji wa mahakama kuu ya Homabay Kiarie Waweru amesema kuwa kuna baadhi ya kesi ambazo zinaweza kusuyluhishwa nje ya mahakama na kuwataka wakaazi kuwahusisha maafiosa wa idara ya mahakama wanapofanya vikao vya kusuluhisha kesi mbali mbali nje ya mahakama ili pawe na rekodi za matukio.
Jaji Kiarie aidha amewaonya maafisa wa idara ya mahakama dhidi ya kujihusisha na ufisadi kwa kuwa wakipatikana watakabiliwa kwa mujibu wa sheria.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































