#Local News

SINA WASHAURI; DUALE AIAMBIA PSC

Waziri wa Ulinzi Aden Duale amesema hana washauri wa kuwasilisha kwa Tume ya Utumishi wa Umma (PSC) ili kusalia kazini kulingana na hatua za kubana matumizi zilizowekwa na Rais William Ruto ili kuakisi hali ya sasa ya uchumi.

Katika waraka uliotumwa kwa Mawaziri wote wa Serikali kutoka kwa Felix Koskei, Mkuu wa Utumishi wa Umma, idadi ya washauri waliopewa kila Katibu wa Baraza la Mawaziri ilirekebishwa kutoka wawili hadi mmoja. Kwa hivyo, mawaziri wote zwalihitajika kuwasilisha majina ya mshauri ili yahifadhiwe kufikia Alhamisi, Julai 11.

Akijibu waraka huo , Duale amefichua kuwa wizara yake haikuwa na washauri kwani maafisa wote walikuwa na mafunzo yanayohitajika ili kutoa ushauri wa kimkakati kwa ofisi yake.

Imetayarishwa na Janice Marete

SINA WASHAURI; DUALE AIAMBIA PSC

GREGG APIGWA KALAMU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *