HATUNA PESA ZAIDI YA MILIONI 391 ZA KUWAPA KAUNTI

Kamati ya bajeti katika bunge la kitaifa imetupilia mbali pendekezo la seneti kuipa kaunti shilingi bilioni 415 Katika bajeti taifa halina uwezo wa kutoa Zaidi ya shilingi 391.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Ndindi Nyoro amesema iwapo wabunge wataidhinisha pendekezo la seneti basi itawalazimu kupunguza bajeti ya hazina ustawishaji maeneo bunge NGCDF.
Ni pendekezo lililoibua mjadala mkali baadhi ya wabunge wakiunga mkono kamati ya bajeti huku wengine wakipinga vikali na kushinikiza kaunti kuongezewa mgao.