KAMATI 7 YABUNIWA KUTENGEZA SRC

Rais William Ruto amebuni kamati yenye wanachama 8 watakaohusika katika kuwasajili makamishna wa tume ya kuratibu mishahara ya wafanyakazi wa umma SRC, baada ya muhula wa miaka 6 wa makamishna waliokuwepo kutamatika.
Wanakamati hao Joshua Wambua, Patrick Mtange, Monica Sifuna, Quresha Abdullahi, Amos Gathecha, Mary Kimonye, Lawrence Kibet na Samuel Kaumba.
Mwenyekiti wa sasa Lynn Mengich na makamishna hao 7 waliingia afisini mwaka 2018 na kisheria kwa makamishna wanaohudumu katika tume za kikatiba na afisi huru hawaruhusiwi kuongezewa muhula mwingine.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa