JUVENTUS KUMTIMUA THIAGO MOTTA, IGOR TUDOR KUCHUKUA NAFASI
Juventus inatarajiwa kumfuta kazi kocha Thiago Motta chini ya msimu mmoja na kumteua Igor Tudor kama mrithi wake.
Tudor atakabiliwa na jukumu la kusaidia klabu kumaliza ndani ya nafasi nne za juu kwenye Serie A ili kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa. Juventus kwa sasa wanashikilia nafasi ya tano huku zikiwa zimesalia mechi tisa.
Chini ya Motta, Juventus imeshinda mechi 18, kutoka sare 16 na kupoteza 8. Mwezi uliopita, waliondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa na Kombe la Italia. Mechi zao mbili za mwisho zilishuhudia vipigo vikubwa kutoka Atalanta na Fiorentina.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































