RISING STARS TAYARI KWA CECAFA

TIMU ya soka ya taifa ya Kenya ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Rising Stars, iko mbioni kushiriki michuano ya CECAFA itakayofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON).
Timu hiyo ilikamilisha maandalizi yao ya mwisho kwa kufanya mazoezi katika Mpesa Academy huko Thika, Kaunti ya Kiambu.
Kocha mkuu Salim Babu alionyesha imani na kikosi hicho huku akieleza kuwa wachezaji wote wako tayari kwa changamoto inayowakabili isipokuwa mmoja ambaye atajiunga na timu hiyo nchini.
Tanzania.Nahodha wa timu hiyo Amos Wanjala ambaye kwa sasa anakipiga Athletic Club Torrellano ya Hispania aliunga mkono kauli ya kocha huyo. matumaini na kusisitiza uungwaji mkono wa timu kutoka kwa serikali na wakufunzi.
Michuano ya kufuzu kwa CECAFA ya U-20 itafanyika kuanzia Oktoba 6 hadi 20. Kenya imepangwa Kundi A, pamoja na wenyeji Tanzania, Rwanda, Sudan na Djibouti.
Mabingwa watetezi Uganda watachuana katika Kundi B, pamoja na Sudan Kusini, Burundi, na Ethiopia.
Imetayarishwa na Nelson Andati