POLISI AMPIGA HAKIMU RISASI MAHAKAMANI

Kizaazaa kimezuka katika mahakama ya Makadara jijini Nairobi baada ya afisa wa polisi wa cheo cha OCS kumpiga risasi na kumjeruhi hakimu mkuu wa mahakama hiyo ambaye jina lake tumelibana, baada ya kutoa uamuzi kwenye kesi inayomhusisha mkewe afisa huyo wa polisi.
Kulingana na kamanda wa polisi eneo la Nairobi Adamson Bungei, afisa huyo amemwandama hakimu huyo nyuma yah ema baada ya uamuzi kwenye kesi hiyo na kutekeleza kisa hicho.
Amesema mshukiwa ni OCS wa kituo kimoja mjini Kisumu, na amesafiri kuhudhuria vikao vya kesi hiyo ambapo alitaka mkewe aacjiwe kwa dhamana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa