#Local News

KOOME NJIA PANDA KUHUSU IEBC

Idara ya mahakama sasa imejipata kwenye njia panda kuhusiana na mchakato wa kubuniwa upya kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC, wakenya wakisubiri kuona iwapo idara hiyo itapuuza agizo lake na kuwaapisha mwenyekiti na makamishna walioteuliwa maajuzi.

Tayari walalamishi Kelvin Omondi na Boniface Mwangi wameelekea mahakamani wakitaka agizo litolewe kuizuia idara hiyo kuwaapisha walioteuliwa, huku wakimshutumu Rais William Ruto kwa kukiuka agizo la mahakama kwa kuchapisha majina ya walioteuliwa licha ya kesi ya kupinga mchakato huo ikiwa bado haijaamuliwa.

Kwenye waraka, walalamishi wamemtaka jaji mkuu Martha Koome kujitenga na zoezi la uapisho.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *