HATUNA IMANI NA JOPO, MAWAKILI WA GACHAGUA
Mchakato wa kusikiliza kesi zinazopinga kutimuliwa kutoka mamlakani kwa naibu rais Rigathi Gachagua umeendelea kuibua hisia, mawakili wake sasa wakitilia shaka uwezekano wa mteja wao kupata haki mbele ya jopo la majaji 3 ambao ni Anthony Mrima, Eric Ogola na Fred Mugambi ambao wameteuliwa kusikiliza kesi hiyo.
Wakiongozwa na wakili Paul Muite, mawakili wa Gachagua wamesema kwamba licha ya majaji hao kudinda kutoa agizo la kuzuia kuapishwa kwa Kithure Kindiki kuwa naibu rais, pia wlaifanya kikao cha dharura Jumamosi bila ufahamu wa mawakili hao.
Aidha, wamesema majaji hao waliandaa kikao cha faragha kujadili ombi lililowasilishwa na mwanasheria mkuu wa serikali na bunge la kitaifa, hofu yao ikijiri saa chache kabla ya kesi hiyo kusikilizwa hapo kesho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































