MAHAKAMA YASITISHAI MCHAKATO WA IEBC
Mahakama kuu imetoa maagizo ya kusitisha kwa muda kuchapisha kwenye gazeti rasmi la serikali majina ya makamishna na mwenyekiti wa tume ya IEBC pamoja na kuapishwa kwao, ingawa ikaliruhusu bunge la kitaifa kuwapiga msasa 7 hao akiwemo mwenyekiti mteule Erastus Ethekon.
Kwenye uamuzi wake, jaji Lawrence Mugambi amewasilisha kesi hiyo kwa mahakama ya upeo ili kubuniwa kwa jopo la majaji watakaosikiliza na kuamua masuala yaliyoibuliwa na walalamishi.
Amebaini kuwa masuala hayo yanahusu mamlaka ya wananchi na hivyo yanastahili kuangaziwa kwa kina.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































