MSWADA WA MAANDAMANO WAPOKEA PINGAMIZI

Mswada uliopendekezwa wa kuifanyia marekebisho sheria kuhusu maandamano umeendelea kupingwa, wa hivi punde kutoa ukosaji wake akiwa ni gavana wa Makueni Mutula Kilonzo Junior ambaye ameutaja kuwa wenye kulirejesha taifa nyuma na kutishia haki za kidemokrasia.
Kupitia taarifa, Mutula amehoji kuwa taasisi kama vile bunge zinafaa kufikiwa na wananchi na wala si kuzuiwa kuzifikia.
Kulingana na mwakilishi wa kike wa Nairobi Esther Passaris ambaye ni mwaasisi wa mswada huo, lengo ni kulinda taasisi hizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa