#Sports

DUKE ABUYA ASHINDA TUZO LA LIGI KUU YA TANZANIA

Mchezaji wa Kimataifa wa Kenya Duke Abuya ameshinda Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya timu yake Young Africans (Yanga) kuwafunga mahasimu wao Simba mabao 2-0 katika mchezo wa Kariokor Derby uliochezwa Jumatano.

Katika mechi ya mwisho ya msimu huu iliyochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, Abuya alikuwa kwenye kikosi cha kwanza na ameshinda ligi yake ya kwanza ya Tanzania tangu avuke mpaka kwa mkopo kutoka Kenya Police FC.

Kiungo huyo mbunifu atafurahi kushinda taji lake la pili la ligi kuu katika ardhi ya kigeni, baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu ya Zambia akiwa na Nkana mnamo 2021.

Kabla ya mechi hiyo, Yanga walikuwa kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na pointi 79, moja bora zaidi ya Simba.

Mabao ya Pacome Zouzoua wa Ivory Coast na Clement Mzize dakika ya 67 na 87 mtawalia ndiyo pekee ambayo Yanga ilihitaji kushinda taji hilo.

Imetayrishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *