NAIROBI THUNDER WAAMBULIA KICHAPO

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Kitaifa ya Kikapu ya Kenya (KNBL) Nairobi City Thunder waliambulia kichapo cha 80-73 dhidi ya wapinzani wao Mamlaka ya Bandari ya Kenya (KPA) katika mpambano wa dhamira ya juu katika Ukumbi wa Michezo wa Nyayo Stadium.
Mechi hiyo ilizikutanisha timu hizo mbili pendwa kushinda taji la msimu huu katika pambano lililojaribu uwezo na werevu wa benchi husika.
Katika pambano lao la kwanza tangu Thunder ilipoizaba KPA 3-0 katika fainali za 2024, Dockers waliibuka kidedea, na kuongoza kwa nguvu 25-16 mwishoni mwa robo ya kwanza.
Waliendeleza kasi hadi mapumziko, wakiongoza 33-24.
Robo ya tatu iliisha kwa mkwamo (18-18), kuweka hatua kwa kipindi cha mwisho cha mvutano.
Zikiwa zimesalia chini ya dakika tatu, KPA waliongoza kwa pointi 11 na walionekana kutawala, hadi Thunder alipomgeukia mshambuliaji nyota Tyler Ongwae kwa kukombolewa.
Imetayarishwa na Nelson Andati