TALANTA YAELEKEA KUKAMILIKA

Ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Talanta jijini Nairobi unaendelea vyema.
Rais William Ruto alikagua maendeleo ya ujenzi Jumanne alasiri na kusema uwanja wa michezo utakamilika kabla ya mwisho wa mwaka ujao tayari kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mnamo 2027.
Uwanja huo utatumika kama uwanja kwa baadhi ya mechi za Afcon.
Rais alieleza Mradi huo utafafanua upya wasifu wa michezo wa Kenya na kusababisha kituo cha kipekee na uboreshaji wa miundombinu kwa Jiji la Nairobi na taifa,
Alibainisha kuwa Kenya ina nia ya kuendeleza na kutekeleza mpango kabambe wa miundombinu ya sekta ya michezo na ubunifu.
Alisema serikali inaboresha miundombinu mbalimbali ya michezo ili kutoa mafunzo bora kwa wanamichezo na wakati huo huo kuendeleza vipaji vya michezo nchini
Imetayarishwa na Nelson Andati